Alexia Super Cup ni mashindano ya soka yaliyoanzishwa mwaka 2023 na Hospitali ya Alexia, Toangoma, Dar es Salaam, kwa lengo la kuhamasisha afya ya jamii. Ni sehemu ya mpango wa hospitali wa kurudisha kwa jamii kupitia burudani ya mpira na huduma za afya bure.






Kaulimbiu yetu ni “Shangwe na Matibabu”: huku mpira, huku afya, huku burudani. Kila mechi inapochezwa, wananchi hupata nafasi ya kupima afya zao na kupata huduma bila malipo.

Tangu kuanza kwake, mashindano haya yamekua kila msimu. Yamevutia mashabiki wengi zaidi, timu nyingi zaidi na wadhamini wengi zaidi. Msimu wa nne mwaka 2026 ulikuwa mkubwa kuliko yote yaliyotangulia, ukishirikisha timu 16 kutoka Temeke, Kigamboni na Mkuranga.
Asanteni wadhamini na washirika wetu
Mafanikio haya ni yenu. Tunawashukuru kwa dhati wadhamini na washirika wote waliotuunga mkono: Equity Bank Tanzania, Hubert Kairuki Hospital, GSM Beverage, Nyumbani Lounge, SokaBet Tanzania, Asas Dairies, Yas Tanzania, Hisense Tanzania, Crown Health Africa, Smart Locks 255 na Geo Green International. Pia tunawashukuru wachezaji, mashabiki na wananchi wote wanaojitokeza kila mwaka.






Karibuni mshirikiane nasi
Tunaendelea kukua, na milango iko wazi kwa kampuni, taasisi na wadau wengine wanaotaka kushirikiana nasi. Mkijiunga nasi, mnaunga mkono michezo, mnasaidia kuokoa maisha na mnaonekana mbele ya maelfu ya wakazi wa Dar es Salaam.
Tukutane msimu ujao! ⚽













