Katika kuendeleza mahusiano tuliyo nayo na jamii na vijana kwa ujumla sasa tumekuja kivingine, ALEXIA SUPER CUP – TUKUTANE VIWANJANI.
Tumetoa nafasi ya timu mbalimbali kushindana kwenye mpira wa miguu, hii yote ni katika kuimarisha afya, kutengeneza mahusiano na kukuza vipaji. Hii ni kwa timu zote zilizopo wilaya ya Mkuranga, Temeke pamoja na Kigamboni.
Mgeni rasmi kwa ajili ya ufunguzi wa mashindano haya atakuwa mbunge wa jimbo la Mbagala, Mh. Abdallah Jafari Chaurembo.
Wote mnakaribishwa.