Kwenye Alexia Super Cup, mpira ulikuwa nusu tu ya hadithi. Nusu nyingine ilikuwa afya. Kila mechi ilipochezwa, madaktari wa Hospitali ya Alexia walikuwa pembeni wakiwahudumia wananchi bila malipo. Hiyo ndiyo maana ya “Shangwe na Matibabu”: huku mpira, huku afya, huku burudani.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Alexia na Mratibu wa Kambi ya Matibabu, Dkt. Seif Salum, alieleza kuwa huduma zingetolewa katika Viwanja vya Masuliza kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni. Huduma zilizotolewa:
Kulikuwa pia na zoezi la uchangiaji damu, lililolenga kusaidia kuokoa maisha ya kina mama, watoto na wagonjwa wengine wanaohitaji damu.
Mratibu Anna Richard Msumule aliwaalika wakazi wa Toangoma, Mandege, Kisemvule, Vikindu, Kongowe, Vijibweni na maeneo mengine ya Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi, akiahidi kuwa msimu huu ungekuwa bora kuliko iliyopita.
Katika hatua zote, kuanzia robo fainali hadi nusu fainali, Hospitali ya Alexia iliendelea kutoa huduma za matibabu bure wakati wa mechi. Mashabiki walipata nafasi ya kupima afya zao huku wakifurahia mpira.



Siku ya fainali, Hospitali ya Alexia na Hubert Kairuki Hospital zilishirikiana kuendesha kambi ya matibabu bure. Huduma zilizotajwa ni:




Mkurugenzi wa Hospitali ya Alexia, Dkt. Humphrey Gatimu, na Mkurugenzi wa Kairuki Hospital, Dkt. Muganyizi Kairuki, walikuwepo kushuhudia huduma hizo. Hospitali hizi mbili zina ushirikiano wa karibu.
Magonjwa mengi, kama saratani, shinikizo la damu na kisukari, hayaonyeshi dalili mapema. Kupima mara kwa mara ndiyo njia bora ya kuyagundua yakiwa bado yanatibika. Kupitia Alexia Super Cup, mamia ya wananchi walipata huduma hizi bila kukatwa hata shilingi.
Hospitali ya Alexia inawashukuru wananchi, wachezaji, wadhamini na wote walioshiriki. Kumbuka: afya ni mtaji, na kupima ni kujali.
#ShangweNaMatibabu #AlexiaHospital #AlexiaSuperCup2026 #AfyaBora #Michezo








