
Jamii ya watu wengi wenye hali ya kipato cha chini wamekua wakipata changamoto ya kumudu gharama za matibabu.
Katika kuliona hilo tumeona tuanzishe mfumo wa kadi maalumu (VOUCHER ZA MATIBABU) zinazo tumika katika vituo vyetu tu, ili kuwawezesha wao kutibiwa kwa gharama ya chini watakayo weza kuimudu kwani wao pia wana haki ya kupata huduma bora za afya.
Vocha izi zilitolewa bure kwa wananchi wote wenye kipato cha chini kupitia wajumbe wa nyumba kumi na serikali za mitaa.