Siku ya tarehe 31 Julai 2021, tulifanya uzinduzi wa hospitali yetu iliyopandishwa hadhi kutoka kuwa kituo cha afya na kuwa hospitali kamili katika wilaya ya Temeke. Hospitali ya Alexia ilianzishwa mwaka 2014 kama zahanati, mwaka 2016 ilipandishwa hadhi kuwa kituo cha afya na Aprili mwaka 2021 ikapandishwa hadhi kuwa hospitali ya ngazi ya wilaya.
Uzinduzi huo ulifanywa na mkuu wa wilaya ya Temeke Mheshimiwa Jokate Mwegelo. Ambaye mara baada ya kuzindua hospitali aliingia ndani ya hospitali na kufanya ziara katika idara mbali mbali zinazotoa huduma kwa wagonjwa.
Pia katika uzinduzi huo, tulitia saini makubaliano ya kibiashara kati ya hospitali yetu na hospitali ya Kairuki ambayo yatawezesha hospitali hizi kushirikiana katika kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi wote.
Pamoja na uzinduzi huo tulitoa huduma mbalimbali bure kama zilivyoorodheshwa hapa chini
Katika jitihada zetu za kuendeleza michezo, tuliandaa shindano la michezo ambalo lilishindanisha timu sita. Mshindi wa kwanza alipata zawadi ya jezi seti mbili. Mshindi wa pili alipata zawadi ya jezi seti moja.