Watoto wa kike wengi wamekua wakikosa masomo kipindi wanapokua katika siku zao. Katika siku ya maadhimisho ya mtoto wa kike duniani mwezi Oktoba 2021, tulishirikiana na Victoria foundation kuchangia taulo za kike kwa watoto wa kike waliopo mashuleni kwani watoto wengi wamekua wakishindwa kumudu gharama za taulo izo. Taulo hizi zitawafikia mabinti wa kike waliopo mkoani Simiyu.