Kunapokuwa kumetokea mabadiliko yasiyo ya kawaida (mutation) kwenye chembe chembe hai zilizopo kwenye mlango wa shingo ya kizazi (Cervix) ndio huitwa saratani ya shingo ya kizazi.
Shingo ya kizazi (cervix) ni kiungo cha mwilini mwa mwanamke kinachopatikana sehemu ya chini ya mfuko wa kizazi (uterus), inayotokezea kwenye uke,
Tafiti za muda mrefu zimeoneshe kwamba maambukizi ya muda mrefu ya kirusi cha Human Papillome (HPV) huchangia kwa kiasi kikubwa. Virusi hewa huambukizwa kwa njia ya kujamiiana japokuwa kinga zetu za asili huwa na uwezo wa kupambana na kudhibiti vizuri hawa. Pale inaposhindikana basi virusi hawa huweza kusbabisha ugonjwa wa saratani.
Kuwa na wapenzi wengi
Kufanya ngono zembe
Kukoma hedhi kwenye umri mkubwa
Matumizi ya mafuta mengi kwenye chakula
Unene kupita kiasi
Uvutaji wa sigara
Unywaji wa pombe kupita kalasi
Kutokufanya mazoezi mara kwa mara
Historia ya saratani ya matiti kwenye familia