Wengi wetu tunajua kuwa mazoezi ni mazuri, lakini tunayaahirisha kwa sababu ya shughuli nyingi. Ukweli ni kwamba mazoezi ni moja ya dawa za bei nafuu na zenye nguvu zaidi tulizonazo. Hayahitaji gharama kubwa, na faida zake huonekana mwilini na akilini.

Mazoezi hupunguza msongo wa mawazo na wasiwasi, na huongeza hali ya furaha na kujiamini. Kutoka jasho kidogo kunaweza kukusaidia kuona siku yako kwa mtazamo mpya.
Michezo si afya tu, bali pia ni mshikamano. Tazama jinsi mpira wa miguu unavyokutanisha vijana, familia na majirani uwanjani. Hiyo ndiyo roho ya Alexia Super Cup, ambako mpira na huduma za afya hukutana ili kuhamasisha jamii. Siku ya ufunguzi wa msimu wa nne, wakimbiaji mbalimbali walishiriki jogging pamoja, wakionyesha kuwa mazoezi yanafurahisha zaidi yakifanywa kwa pamoja.

Kwa mujibu wa mwongozo wa Shirika la Afya Duniani (WHO):


Mazoezi ni muhimu, lakini hayachukui nafasi ya vipimo vya afya. Kama una ugonjwa wa muda mrefu, una umri mkubwa, au hujafanya mazoezi kwa muda mrefu, wasiliana na daktari kabla ya kuanza mazoezi mazito. Kupima mara kwa mara shinikizo la damu, sukari na magonjwa mengine hukusaidia kujua hali yako halisi.
Afya ni mtaji, na mazoezi ni uwekezaji wenye faida kubwa. Huhitaji kuwa mwanamichezo wa kitaaluma ili kunufaika. Vaa viatu vyako, toka nje, na anza leo.








