• Home
  • Medical Services
  • About
    • Overview
    • Letter From the CEO
  • Health Tips
  • News & Updates
    • News
    • CSR Activities
    • Events
  • Contacts
    • Locations & Directions
    • Patients & Visitors Guide
    • Useful Phone Numbers
    • Book an Appointment
  • Emergency: +255 786 842 339
  • COVID-19 Testing
  • COVID-19 Vaccination
  • COVID-19 Testing Appointment
  • COVID-19 Vaccination Appointment
  • Home
  • Medical Services
  • About
    • Overview
    • Letter From the CEO
  • Health Tips
  • News & Updates
    • News
    • CSR Activities
    • Events
  • Contacts
    • Locations & Directions
    • Patients & Visitors Guide
    • Useful Phone Numbers
    • Book an Appointment

  • Emergency: +255 786 842 339
  • Home
  • Medical Services
  • About
    • Overview
    • Letter From the CEO
  • Health Tips
  • News & Updates
    • News
    • CSR Activities
    • Events
  • Contacts
    • Locations & Directions
    • Patients & Visitors Guide
    • Useful Phone Numbers
    • Book an Appointment

Saratani ya Mfuko wa Mayai ya Mwanamke (Ovarian Cancer)

By admin  Published On September 18, 2025

Umuhimu wa Uchunguzi wa Saratani ya Mfuko wa Mayai (Ovarian Cancer)

Saratani imekuwa moja wapo ya magonjwa yanayoua wanawake wengi, na saratani ya mfuko wa mayai inachangia pakubwa katika vifo hivyo, ikiwa ni moja ya saratani tano zinazoongoza kwa vifo vya wanawake. Ni vigumu kugundua saratani ya mfuko wa mayai katika hatua za awali. Kwa hiyo, wanawake wanahitaji kupata elimu na kuchunguzwa mapema ili kuzuia saratani hiyo kuwa mbaya na ngumu kutibika.

Dalili za Saratani ya Mfuko wa Mayai (Ovarian Cancer)

Dalili za awali za saratani ya mfuko wa mayai mara nyingi ni ngumu kugundulika. Hata hivyo, Daktari Kitange anashauri wanawake waende hospitalini wakiona dalili zifuatazo:

  • Mzunguko wa hedhi usio mzuri (Irregular menstrual cycle)
  • Maumivu ya chini ya tumbo: Maumivu haya hayahusiani na hedhi
  • Kuhisi tumbo linajaa haraka: Hata kabla ya kumaliza kula chakula kidogo, tumbo linahisi kujaa
  • Kukojoa mara kwa mara
  • Kushindwa kupata choo kikubwa

Uchunguzi na Hatua za Kuchukua: Hakuna vipimo maalum vya awali vinavyoweza kuthibitisha moja kwa moja saratani ya mfuko wa mayai. Hata hivyo, Daktari Kitange anashauri wanawake wenye dalili hizo wafike hospitalini kwa uchunguzi. Ultrasound ni moja ya vipimo vinavyotumika kugundua uvimbe katika mfumo wa uzazi.

Kundi Lililo Kwenye Hatari (Risk Group) Ya Kupata Saratani ya Mfuko wa Mayai

Wanawake walio katika hatari kubwa ya kupata saratani hii ni wale ambao

  • Wana shida ya uzazi.
  • Wamekaa kwa muda mrefu bila kupata watoto.
  • Wana umri mkubwa bila kuwa na watoto.
  • Wanafuatilia uchunguzi kutokana na kushindwa kupata mimba.

Wanawake wenye umri mkubwa wanashauriwa kwenda hospitalini kwa uchunguzi wa saratani ya mfuko wa mayai. Daktari Kitange anawakaribisha wanawake hospitalini Alexia kupata huduma za uchunguzi na matibabu yanayostahili kabla saratani haijafika katika hatua ngumu kutibika. Huduma hizi zinapatikana hospitalini hapo kila siku ya Jumanne. Piga simu +255 677 006 700 kwa maelezo zaidi kuhusu ratiba ya daktari

Unaweza kutazama video kamili hapa chini


Fainali za Alexia Super Cup 2025
Previous Article

FOR PATIENTS

Health Tips
Patient & Visitor's Guide
Book an Appointment
Billing & Payments
Medical Specialists

ABOUT US

Overview of Our Work
Locations & Directions
News & Updates
Events
Job Opportunities

CONTACT US

+255 655 842 339
+255 736 842339
info@alexiamedical.co.tz
Member of
Accepted Payments
Accepted Insurance Providers
insurance – 4
insurance – 7
insurance – 10
insurance – 5
insurance – 6
insurance – 1
insurance
insurance – 3
uap-mutual
  • Privacy Policy
  • Terms of Use