
Fainali ya Alexia Supercup mwaka 2025 imekuja kivingine kwa kujikita kwenye kutoa huduma za afya bure siku nzima huku michezo na burudani ikiendelea. Jumamosi ya tarehe 13/09/2025 katika viwanja vya Masuliza Toangoma kulifana sana. Mgeni mualikwa alikuwa Bw. Kakulu Burchad Kakulu, mgombea wa kiti cha ubunge jimbo la Mbagala.
Fainali ilikuwa ni kati ya timu ya Mzinga FC na Goroka FC, ambapo timu ya Goroka iliibuka kidedea na kuondoka na kitita cha fedha taslimu shs milioni tatu za kitanzania.
Pia kulikuwepo wageni kama Bw. Hassan Ahmed, mtayarishaji na mwandishi wa habari za michezo, Bondia Mandonga Mtu Kazi. Upande wa burudani alikuwepo Meja Kunta pamoja na Angel Nyigu, ambao walitoa burudani ya kufa na shoka.
Pia kulikuwepo mechi ya kirafiki kati ya Alexia FC pamoja na timu kutoka hospitali ya Kairuki ambapo timu ya Kairuki iliibuka kidedea kwa goli 2-1.
Picha zaidi kutoka kwenye eneo la tukio