Pamoja na kujali afya za wagonjwa wetu hospitali ya Alexia inajali usalama wa wafanyakazi wake. Kama hospitali tunafanya jitihada za kuhakikisha kuwa wafanyakazi wanakuwa na uwezo wa kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoweza kujitokeza wakati wa kazi.
Katika kulizingatia hili wafanyakazi wa hospitali ya Alexia wamepata mafunzo kutoka kwa jeshi la zimamoto na uokoaji Dar es salaam. Kupitia mwakilishi wa jeshi la zimamoto na uokoaji wafanyakazi wamejifunza namna mbalimbali za kukabiliana na majanga ya moto.