
Saratani imekuwa moja wapo ya magonjwa yanayoua wanawake wengi, na saratani ya mfuko wa mayai inachangia pakubwa katika vifo hivyo, ikiwa ni moja ya saratani tano zinazoongoza kwa vifo vya wanawake. Ni vigumu kugundua saratani ya mfuko wa mayai katika hatua za awali. Kwa hiyo, wanawake wanahitaji kupata elimu na kuchunguzwa mapema ili kuzuia saratani hiyo kuwa mbaya na ngumu kutibika.
Dalili za awali za saratani ya mfuko wa mayai mara nyingi ni ngumu kugundulika. Hata hivyo, Daktari Kitange anashauri wanawake waende hospitalini wakiona dalili zifuatazo:
Uchunguzi na Hatua za Kuchukua: Hakuna vipimo maalum vya awali vinavyoweza kuthibitisha moja kwa moja saratani ya mfuko wa mayai. Hata hivyo, Daktari Kitange anashauri wanawake wenye dalili hizo wafike hospitalini kwa uchunguzi. Ultrasound ni moja ya vipimo vinavyotumika kugundua uvimbe katika mfumo wa uzazi.
Wanawake walio katika hatari kubwa ya kupata saratani hii ni wale ambao
Wanawake wenye umri mkubwa wanashauriwa kwenda hospitalini kwa uchunguzi wa saratani ya mfuko wa mayai. Daktari Kitange anawakaribisha wanawake hospitalini Alexia kupata huduma za uchunguzi na matibabu yanayostahili kabla saratani haijafika katika hatua ngumu kutibika. Huduma hizi zinapatikana hospitalini hapo kila siku ya Jumanne. Piga simu +255 677 006 700 kwa maelezo zaidi kuhusu ratiba ya daktari
Unaweza kutazama video kamili hapa chini