Hospitali Alexia katika kuthamini mchango wa michezo kwa vijana na kushirikiana na Hatua Initiative wametoa msaada wa vifaa vya michezo. Michezo ni moja kati ya njia nzuri za kujenga afya na sisi kama hospitali kazi yetu kuu ni kuhakikisha jamii kwa ujumla wanakua na afya na kuwa na mienendo inayosaidia kutunza afya zao.