News

Alexia Health Center is now rated 4 stars in BRN (Board Of Registered Nursing),  We are so proud of our team and all the effort they put on.

Upungufu wa damu (anaemia)

hutafsiriwa kama kupungua kwa kiwango cha hemoglobin katika damu damu chini ya kiwango kinachokubalika kiafya. Kiwango cha kawaida cha haemoglobin (Hb) katika mwili wa binadamu ni kati ya gramu 12 mpaka 14 kwa kila mililita ya damu. Hata hivyo shirika la afya duniani (WHO) linatambua kiwango cha mpaka 11gm/mililita kuwa cha kawaida kwa mama mjamzito. Hivyo basi mjamzito mwenye kiwango chochote cha haemoglobin chini ya 11 gm/mililita hutafsiriwa kuwa na upungufu wa damu. Hata hivyo nchi nyingi hasa zinazoendelea hutambua kiwango cha mpaka gramu 10 kwa mililita kuwa ni upungufu wa damu kwa mjamzito.

Kwa mjamzito anayehudhuria kliniki kwa mara ya kwanza, upungufu wa damu kipindi cha ujauzito humaanisha kiwango cha hemoglobin chini ya <11.0 g/dL, na mimba inapofikisha wiki 28 upungufu wa damu hutambuliwa iwapo hemoglobin itashuka na kuwa chini ya 10.5 g/dL.

Daktari mmoja aitwaye Mackod, alipitia makala nyingi za afya ili kuweza kutambua visababishi vya vifo ambayo havitokani na umri au nasaba ya kiasili (Genetic), na akagundua mambo tisa ambayo yanasabisha vifo ambavyo vingeweza kuzuilika. Mambo hayo tisa ni; uvutaji wa sigara, unywaji wa pombe, kutofanya wa mazoezi, lishe duni, wadudu kama bakteria na virusi, ajali, tabia za ngono za kupita kiasi bila kinga, vita na madawa ya kulevya.

Katika makala hii ningependa kuzungumzia juu ya ufanyaji wa wazoezi na hasa wakati bora wa kufanya mazoezi. Mazoezi ni muhimu sana kwa ajili ya kupunguza mafuta ya ziada mwilini, tafiti zinaonesha kuwa asiyefanya mazoezi, madhara anayopata ni sawa na mtu anayevuta tumbaku.

 

Ultrasound ni chombo ambacho kimekuwa kikitumiwa na madaktari wengi sehemu mbalimbali duniani kwa ajili ya kuchunguza matatizo mbali mbali yaliyo ndani ya mwili wa mgonjwa.

Mojawapo ya matumizi maarufu ya chombo hiki kwa wanawake ni utambuzi wa jinsi mtoto alivyokaa tumboni mwa mama mjamzito,kuchunguza umbo la mfuko wa uzazi, matatizo katika mfumo wa uzazi na pia kuangalia iwapo kiumbe kilichopo ndani ya tumbo la mama mjamzito ni hai ama la.

Hivi karibuni huko nchini Uingereza, madaktari wamebuni kipimo cha Ultrasound kinachoweza kugundua kansa ya mfuko wa kizazi mapema kabla ya hata dalili hazijaanza kujitokeza kwa mgonjwa. Kipimo hicho kina uwezo wa kugundua kansa ya mfuko wa uzazi kwa mwanamke ikiwa katika hatua za awali kabisa kabla hata ya dalili zake kuanza kujitokeza rasmi.

Utangulizi

Saratani ya shingo ya kizazi ni saratani inayoongoza kwa kusababisha vifo vya wanawake wengi duniani. Inakadiriwa kuwa asilimia 85 ya vifo hivi hutokea katika nchi zinazoendelea. Kwa Tanzania, wastani wa wanawake 6,241 huugua saratani hii kila mwaka, ambapo 4,355 kati yao hufa, hii ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la afya duniani (W.H.O) ya mwaka 2010

Saratani ya shingo ya kizazi ndio saratani ya kwanza kwa wanawake nchini Tanzania, na Saratani namba moja kwa wanawake walio kati ya umri wa miaka 15 hadi 44. Tanzania ina wanawake milioni 10.97 walio na umri wa miaka 15 na kuendelea, ambao wako kwenye hatari kubwa ya kupata saratani hii. Kwa afrika mashariki, asilimia 33.6 ya wanawake wote, wanasadikiwa kuwa na virusi aina ya human papilloma virus ambavyo ndio visababishi vya ugonjwa huu.

Menu